salaam,

Twakukaribisha kwenye mtandao huu. Katika nyakati hizi za taabu twahitaji mwongozo na majibu. Mtandao huu ni kwa ajili yako wewe! Waweza kupokea na kunakili kitabu cho chote au makala yo yote.

Vitabu vya bure.

Asante Sana, R.M. (Rudy) Harnisch

 

Ujumbe wa leo

"Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, yeye ajaye atakuja, wala hata kawia" (Waebrania 10:37)

Tumaini kuu

Katikati ya shida na majaribu, dhiki na mateso, ugonjwa na njaa, kukatishwa tamaa na kudharauriwa, uhusiano uliovunjika, uchungu na kukata tamaa. lipo tumaini kuu. Unaweza kupata faraja na kuanza maisha upya iwapo tu utamwangalia mwokozi. Mungu anasema "Niangalieni mimi, mkaeokolewe, enyi ncha zote za dunia, maana mimi ni Mungu, hapana mwingine" (Isaya 45:22)

Usingizi katikati ya ving'ora?

Bila shaka yoyote dunia hii inaelekea mwisho wake, sikiliza redio, angalia luninga, tembelea mitandao ya kijamii vyote hivi vinatoa mwangwi wa ving'ora (dalili) vya kurudi kwake Bwana. Yesu alisema, " Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa patika siku zake Mwana wa Adamu." (Luka 17:26)

Soma zaidi